Ujenzi Mbadala

Compressed Stablized Interlocking Earth Blocks (CSIEB) ni matofali zinazotumika kujengea majengo yenye ubora na kwa bei nafuu. Udongo unachanganishwa na chokaa au saruji na inagandamizwa ndani ya mashine kupata matofali yanayounganishana. Baada ya kuauka kwa mwezi mmoja, matofali haya yako tayari kwa ujenzi.  Kwani zinaunganishana hamna haja kutumia saruji katikati ya matofali na inapunguza gharama na muda wa kujenga.