Kilimo Mbadala

Jamii zetu wanatumia mbinu bora ya kulima bustani ndogo inayozidisha upatikanaji wa matunda na mbogomboga kwa afya bora.

Bustani za "Biointensive"

Kutayarisha bustani ya "biointensive" unalima chini zaidi kupunguza ushindani katikati ya mizizi. Hii inazidisha idadi ya mbogamboga kwenye eneo ndogo.

Bustani Kwenye Polo

Bustani Kwenye Polo zinasaidia jamii ambao hawana eneo au maji ya kutosha. Unatia udongo kwenye polo yako na pembeni ya polo unakata duara nyingi ndogo. Unapanda mbegu ndani ya duara hizi. Kwani mbegu zinapandwa wima, maji kidogo inatosha kuroesha mbegu zote.

Bustani za Ufunguo

Bustani za ufunguo ni duara yenye nafasi kidogo kilichokatwa kwa binadamu kusimama. Kwani udongo uko juu, mizizi hazishindani na unaweza kupanda mbogomboga nyingi kwenye eneo ndogo.

Compost

Compost ni mbolea kutoka taka za nyumbani ambazo siyo plastik, metali wala glasi. Unaiweka sehemu maalum na kila wiki tatu unaigeuza. Wadudu wanakula taka hii na baada ya wiki sita hadi nane utapata mbolea.